• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini baadhi ya samaki wanaonekana kama wanataka kujiua?

    (GMT+08:00) 2016-07-27 14:51:19

    Wafugaji wa samaki aina ya salmon wametambua jambo la ajabu kwamba katika bwawa moja, samaki wengi wanakula na kukua, lakini wengine hawali wala kuogelea, wanaonekana kama wanataka kujiua kwa kujinyima chakula.

    Watafiti kutoka Norway, Denmark na Uholanzi wametafiti jambo hili, na kugundua kuwa samaki hao si kama tu wana sura tofauti, bali pia utoaji wa kemikali ndani ya miili yao ni tofauti.

    Kwanza, damu ya samaki wasiotaka kula ina Cortisol nyingi, ambayo inamaanisha wanakabiliwa na shinikizo kubwa kuliko wengine.

    Pili, ubongo wa samaki wasiotaka kula siku zote una Serotonin nyingi, ambayo ni dalili ya mfadhaiko, Binadamu akiwa na kemikali hii nyingi ubongoni, inamaanisha kuwa ana hatari kubwa ya kujiua.

    Je, kwanini samaki hao wana dalili ya mfadhaiko?

    Samaki wamezoea kuishi kwenye mazingira ya asili tangu zamani, wakati wanapofugwa na binadamu mabwawani, hukabiliwa na mashinikizo mbalimbali yakiwemo msongamano mkubwa na kushtushwa na binadamu mara kwa mara. Baadhi yao wana uwezo mkubwa wa kukabiliana na mazingira mapya, lakini wengine hawana.

    Basi utafiti wa samaki hao una umuhimu gani? Kwanza, utawasaidia wafugaji kuchagua samaki wanaofaa kufugwa na kuongeza uzalishaji. Pili, unawasaidia wanasayansi kutafiti ubongo wa binadamu na kutafuta tiba ya mfadhaiko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako