• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • East Africa: Wanawake wa biashara kutoka EAC waomba usaidizi zaidi

    (GMT+08:00) 2016-07-27 20:00:55
    Serikali za afrika kusini zimeombwa kutoa msaada zaidi kwa wanawake katika biashara ili kuweza kuimarisha ujasiriamali na kuhakikisha usawa na maendeleo endelevu.

    mwenyekiti wa Wanawake katika Biashara katika chama cha kitaifa cha wafanyibiashara na Viwanda (KNCCI)Mary Muthoni,amesema wajasiriamali wanawake wanauwezo mdogo wakupata mikopo nafuu, na ukosefu wa ujuzi kwa baadhi yao.

    Aidha amesema changamoto hizi zinazuia jitihada za wanawake kujiingiza katika biashara ya mpakani.

    Hivyo ni muhimu kwa serikali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuelewa changamoto hizi na kutengeneza sera ambayo itatengeneza mazingira bora na rahisi kwa wanawake kufanya biashara.

    Aliongeza kuwa kuna haja ya mafunzo kwa wanawake na ujuzi kuweza kuwasaidia kujisimamia na kuendesha biashara ya mpakani vizuri.

    Muthoni alikuwa akiongea katika mkutano wa wanawake na biashara wa kenya na rwanda mjini kigali jana.

    Mkutano ambao ulivutia zaidi ya wanawake 100 wajasiriamali kutoka Kenya na Rwanda, uliandaliwa na Shirikisho la Sekta Binafsi (PSF) na KNCCI-sekta ya biashara ya Wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako