• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wasema taarifa kuhusu vurugu za kingono Sudan Kusini zinasikitisha

    (GMT+08:00) 2016-07-28 09:59:24
    Matukio ya vurugu za kingono dhidi ya raia yameendelea kuripotiwa nchini Sudan Kusini, tangu mapigano yalipuke mjini Juba.

    Tume ya umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, imesema inaendelea kupokea ripoti za matukio ya ubakaji na ubakaji wa makundi, unaofanywa na wanajeshi wenye sare, na watu wasiokuwa na sare, ikiwa ni pamoja na ubakaji dhidi ya watoto, karibu na nyumba ya umoja wa mataifa mjini Juba.

    Msemaji wa Umoja wa mataifa Bw Farhan Haq amesema tume ya umoja wa mataifa imeimarisha doria ili kuwalinda raia, ndani na karibu ya maeneo ya umoja wa mataifa ya ulinzi wa raia.

    Maofisa wa umoja wa mataifa wamesema hali ya Sudan Kusini bado ni tete, tangu yalipotokea mapambano kati ya wanajeshi wa serikali na wa upinzani, na kusababisha vifo vya watu 272, ikiwa ni pamoja na raia 33.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako