• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachunguzi wa amani nchini Sudan Kusini wajadili mgogoro wa kisiasa nchini humo

    (GMT+08:00) 2016-07-28 10:08:18

    Wachunguzi wa amani nchini Sudan Kusini wamefanya mazungumzo na pande mbalimbali za mgogoro nchini humo baada ya rais Salva Kiir wa nchi hiyo kumwondoa madarakani makamu wake wa kwanza Riek Machar.

    Tume inayosimamia na kutathmini utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa Agosti mwaka jana, imesema inafuatilia kwa makini maendeleo ya kisiasa nchini Sudan Kusini.

    Mwenyekiti wa tume hiyo Bw. Festus Mogae ametoa taarifa akisema, amefanya mazungumzo na rais Kiir na Bw Taban Deng Gai ambaye ameteuliwa kuwa makamu wa kwanza wa rais, pamoja na maofisa wawili wa chama cha SPLM/IO kinachoongozwa na Bw Machar. Kwa mujibu wa tume hiyo, rais Kiir ameeleza utayari wa kufikiria kuwekwa vikosi vya kulinda amani ya kikanda nchini humo kulingana na mapendekezo yaliyotolewa na mkutano uliopita wa wakuu wa Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako