Naibu katibu wa sekretariati ya Kamati ya maandalizi ya maoneysho hayo Bw. Tian Chuan amesema, idadi ya nchi zinazotaka kushirikiana na China katika kuandaa maonyesho hayo imeongezeka zaidi. Licha ya Cote d'Ivoire, nchi kama Afrika Kusini, Nigeria, Kenya, na Ethiopia zote zimeonesha nia kubwa ya kushiriki kwenye maandalizi ya maonesho hayo, na wajumbe wa nchi hizo watahudhuria maonyesho ya mwaka huu.
Mkuu wa ofisi ya mambo ya maonyesho hayo Bw. He Zuoxian amesema, maonesho hayo yataweka mabanda 4,600 yenye eneo la jumla mita za mraba laki moja, na kwamba nchi zaidi ya 20 zikiwemo Russia, Japan, Ujerumani na Uturuki, zimethibitisha kushiriki kwenye maonyesho hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |