• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japan yakuza viazi visivyo na sumu

    (GMT+08:00) 2016-07-29 09:53:10

    Viazi vikitoa miche vitakuwa na sumu, na watu wakila viazi hivi wataumwa. Hivi karibuni kikundi cha utafiti cha Japan kimekuza viazi visivyo na sumu.

    Viazi vinazalisha kemikali mbalimbali aina ya Glycoalkaloids, ambazo asilimia 95 ni alfa-Solanine na alfa-Chaconine. Kemikali hizi nyingi ziko ndani au kando ya miche. Hivyo usiwe na wasiwasi unapokula viazi vilivyotoa miche. Lakini viazi vikitoa miche, ni hatari, miligramu 400 za Solanine zitamwua mtu mzima.

    Watafiti kutoka Taasisi ya Fizikia na Kemikali ya Japan RIKEN na Chuo Kikuu cha Osaka wamegundua kuwa jeni mbili za PGA1 na PGA2 za viazi zinahusiana na uzalishaji wa kemikali za alfa-Solanine na alfa-Chaconine. Baada ya kuzuia jeni hizi zisifanye kazi, uzalishaji wa kemikali hizi unapungua kwa kiasi kikubwa, lakini mchakato wa kukua na kukomaa hautaathiriwa.

    Viazi vinatoa miche miezi kadhaa baada ya kuvunwa, hivyo haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu sana. Watafiti wamegundua kuwa jeni hizi zikizuiliwa, viazi vitachelewa kutoa miche.

    Utafiti huo utaongeza usalama wa viazi na kuwasaidia watu kuhifadhi viazi kwa urahisi zaidi. Ripoti ya utafiti huo imetolewa kwenye tovuti ya gazeti la Fiziolojia ya Mimea la Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako