• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la Vijana wa China na Afrika kwa Mwaka 2016 laendelea mjini Guangzhou

    (GMT+08:00) 2016-08-03 16:34:13

    Tamasha la Vijana wa China na Afrika kwa Mwaka 2016 linaendelea kufanyika mjini Guangzhou, ambapo vijana 188 kutoka nchi 18 za Afrika na wenzao 200 kutoka China wamekusanyika kwa pamoja ili kuongeza maelewano kati yao.

    Mwezi Disemba mwaka jana, mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC ulifanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Pande hizo mbili zilikubaliana kujenga uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa kina na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, ikiwemo kutembeleana kati ya vijana na kuandaa kwa zamu "Tamasha la Vijana wa China na Afrika". Naibu mkuu wa Shirikisho la Urafiki na Nje la China Bibi. Lin Yi anasema kufanyika kwa shughuli hizo huko Guangzhou ni kutekeleza makubaliano hayo.

    "Tunatarajia kuwa vijana wa Afrika wanaweza kuelewa zaidi utamaduni wa kichina kupitia kutembelea vyuo vikuu na kushiriki kwenye huduma za kujitolea, kuwafahamisha kuhusu uchumi na teknolojia za China kupitia kutembelea kampuni, na kutimiza ndoto ya pamoja ya vijana wa China na Afrika kupitia kushiriki kwenye kongamano la ujasiriamali. Tuna matumaini ya dhati kuwa vijana wa Afrika wanaweza kujenga urafiki na wenzao wa China, na pia vijana wa China wanaweza kuifahamu na kuipenda Afrika."

    Mjumbe wa vijana wa Afrika ambaye ni mshauri wa rais wa Gabon A.J. Denis Ayenoe ameishukuru China kwa kutoa jukwaa la mawasiliano kwa vijana wa China na Afrika na kusema kuwa vijana wa Afrika wako pamoja na wenzao wa China na kuchangia maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Anasema,

    "Afrika na China zina urafiki mkubwa wa jadi, Afrika ni eneo linaloibuka upya kimaendeleo na lina fursa nyingi na nguvu za kibiashara, pia ni eneo zuri kwa uwekezaji. Katika miaka ya hivi karibuni, China imeongeza uwekezaji wake barani Afrika, ambao umehimiza maendeleo na ujenzi wa Afrika, na tunatarajia kuwa, China itapanua uwekezaji wake zaidi na kutoa msaada wa kiteknolojia kwa Afrika."

    Babikiri Mai Ibrahim Hassan ni mwanadiplomasia kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan, na anashangazwa na kasi kubwa ya maendeleo ya China na ana hamu ya kujua kila kitu nchini China.

    "Tamasha hilo limetupatia fursa ya kuja China, kuifahamu China na vijana wa China na Afrika wanaweza kuwasiliana uso kwa uso kwenye tamasha hilo. Kasi ya maendeleo ya China imenishangaza na kunivutia. Natarajia kuwa siku za baadaye za China zitakuwa nzuri na urafiki kati ya China na Afrika utadumu milele!"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako