• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Yanga Hans van Pluijm aahidi makubwa dhidi ya MO Bejaia

    (GMT+08:00) 2016-08-04 08:27:46

    Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Hans van Pluijm, amepanga kurejesha imani na furaha iliyopotea kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kuhakikisha wanawafunga MO Bejaia katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika. Kocha huyo mholanzi amekiri kuwa matokeo mabaya wanayoendelea kuyapata yanawakatisha tamaa mashabiki na kusababisha imani na timu yao kupungua. Aidha, kocha huyo alisisitiza kuwa amejipanga kuwafurahisha mashabiki wake ili wasiendelee kuvujika moyo na kukosa imani na timu yao.

    Yanga ipo mkiani katika Kundi A, ikiwa na pointi moja, imepoteza michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja kati ya michezo minne iliyocheza. Klabu hiyo inatarajia kuvaana na MO Bejaia Agosti 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano ikiwa mchezo wa kwanza waliambulia kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa waarabu hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako