• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yasanifu roboti mpya ya vita

    (GMT+08:00) 2016-08-08 10:24:18

    Kiwanda cha silaha cha Degtyarev na Mfuko wa utafiti katika mustakabali wa Russia vimesanifu kwa pamoja roboti ya vita ya "Nerekhta-2".

    Roboti hii inayofanana na kifaru kidogo ina urefu wa mita 2.5, upana wa mita 1.6 na kimo cha mita 0.9, na uzito wake ni tani 1 hivi.

    Roboti hii inaweza kufanya doria, kuchunguza, kusaidia mapambano, kufanya mawasiliano, na kusafirisha watu na vitu. Ina bunduki moja nyepesi yenye kipenyo cha milimita 7.62 na bunduki moja nzito yenye kipenyo cha milimita 12.7. Watafiti pia wanapanga kuweka mzinga mdogo kwenye roboti hii.

    Askari wanaweza kuwasiliana na roboti hii kwa remote kwa umbali wa kilomita 3. Pia inaweza kuendeshwa kwa maneno au ishara ya mikono. Askari akitaka roboti hii kumsaidia, anatakiwa kupunga silaha yake kwa njia maalum, baadaye roboti inafyatulia risasi kitu au mtu aliyelengwa.

    Mchana roboti hii inaweza kutambua shabaha iliyoko umbali wa kilomita 5 kutoka mahali ilipo kwa darubini, na usiku inaweza kutambua shabaha iliyoko kilomita 4 kwa kifaa cha kuonea usiku.

    Roboti hii ina injini yenye nguvu kubwa, na inaweza kuendeshwa kwa kasi ya kilomita 32 kwa saa. Inapofanya kazi ya usafirishaji, inaweza kubeba vitu vyenye uzito wa kilo 700.

    Askari mmoja anaweza kuziongoza roboti 18 kufanya kazi kwa pamoja kwa remote moja tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako