• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba yaiadhibu AFC Leopard 4-0

    (GMT+08:00) 2016-08-09 10:08:34

    Simba wameibuka na ushindi wa goli 4-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya Kenya uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

    Mechi ihiyo ilikuwa ni ya maadhimisho ya miaka 80 ya klabu hiyo ya Simba.

    Kocha Joseph Omog aliwatumia wachezaji wake nyota wa kimataifa kama sehemu ya kuwatambulisha akiwemo mshambuliaji mpya kutoka Burundi Laudit Mavugo aliyeingia kipindi cha pili.

    Ibrahim Ajibu alifanikiwa kufunga goli dakika ya 38 na 60 na baadae Shiza Kichuya alipachika goli la tatu dakika ya 66 baada ya kupokea PASI safi kutoka Laudit Mavugo ambaye pia alihitimisha ushindi wa Simba kwa kupachika goli la nne dakika ya 84.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako