• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Li Zhaoxing akutana na waziri mkuu wa zamani wa Tanzania Salim Ahmed Salim na rais wa zamani wa nchi hiyo Benjamin Mkapa

  (GMT+08:00) 2016-08-09 19:50:50

  Mkurugenzi wa Shirikisho la diplomasia ya umma la China Bw. Li Zhaoxing ambaye yuko ziarani nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa Baraza la diplomasia ya umma kati ya China na Afrika, jana alikutana na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Bw. Salim Ahmed Salim na rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Benjamin Mkapa.

  Bw. Li Zhaoxing amesema kukuza ushirikiano na mshikamano na nchi za Afrika ni msingi muhimu wa sera ya kidilpomasia ya China, na pia ni chaguo la kimkakati ambalo China imelifuata kithabiti kwa muda mrefu. Bw. Li pia ameshukuru uungaji mkono wa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kwa China kwenye masuala yanayohusiana na maslahi muhimu ya China.

  Kwa upande wao, Bw. Salim na Bw. Mkapa wamesema, Tanzania siku zote inatilia maanani urafiki kati yake na China, na uzoefu wa historia umethibitisha kuwa urafiki kati ya nchi hizo mbili ni urafiki wa kweli unaojengwa kwenye msingi wa kusaidiana na kuheshimiana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako