• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dhoruba ya jua ilikaribia kusababisha vita vya nyuklia katika karne iliyopita

    (GMT+08:00) 2016-08-11 16:14:25

    Wakati wa vita baridi, Urusi ilipeleka makombora nchini Cuba, na kukaribia kusababisha vita vya nyuklia kati ya Urusi na Marekani. Lakini watu wachache wanajua kuwa wakati huo, dhoruba kubwa ya jua pia ilikaribia kusababisha vita vya nyuklia kati ya pande hizo mbili. Tukio hili limefichuliwa tarehe 9 na watafiti kwa mara ya kwanza.

    Upepo wa jua ni mkondo mfululizo wa vitu vidogo vidogo unaotoka kwenye jua, hasa protoni, elektroni na viini vya Helium zenye kasi kubwa, wakati upepo huo unapokuwa mkubwa sana, unaitwa dhoruba ya jua.

    Katika miaka ya 60 karne iliyopita, baadhi ya ndege za kivita za Marekani zikibeba makombora ya nyuklia ziliruka angani siku zote, ili kuzuia Urusi isianzishe vita vya nyuklia ghafla. Tarehe 23 Mei mwaka 1967, dhoruba kubwa ya jua iliathiri vibaya rada za jeshi la Marekani katika ncha ya kaskazini ya dunia ambazo zilitumiwa kuchunguza makombora ya Urusi. Makamanda wa jeshi walidhani rada hizi zilizuiliwa na Urusi na kuchukulia kitendo cha kuzuia rada zote ni ishara ya kuanzisha vita, na waliziamrisha ndege za kivita kujitayarisha kushambulia. Kwa bahati nzuri jeshi la Marekani lilitambua athari ya upepo wa jua kwa vifaa vya elektroniki duniani, na kutoanzisha vita.

    Tukio hili limefichuliwa tarehe 9 na watafiti wa Chuo Kikuu cha Colorado cha Marekani baada ya kuwahoji wadau wa jeshi la Marekani na kusoma nyaraka husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako