• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la ardhi kilimo China bado liko juu ya "kikomo cha chini"

    (GMT+08:00) 2016-08-11 20:32:32

    Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana eneo la ardhi inayofaa kwa ajili ya kilimo nchini China lilikuwa zaidi ya hekta milioni 135, na kuwa juu ya kikomo cha chini kilichowekwa na serikali.

    Wizara ya Ardhi na Raslimali imesema China inatakiwa kuhifadhi walau hekta milioni 124 za ardhi inayofaa kwa shughuli za kilimo hadi ifikapo mwaka 2020, kwa kuwa karibu nusu ya wachina ni wakulima, na usalama wa chakula ni moja ya changamoto kubwa kwa China.

    Takwimu za mwezi Aprili za wizara hiyo zinaonyesha kuwa, mwaka jana hekta zipatazo laki 3 za kilimo zilipotea kutokana na shughuli za ujenzi, majanga, utunzaji wa mazingira na mageuzi ya kilimo, ambapo hekta laki 2.5 za mashamba mapya zilianzishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako