• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zinatarajia mkutano wa G20 utajadili changamoto za dunia

    (GMT+08:00) 2016-08-16 16:43:08

    Nchi za Afrika zina matarajio makubwa kuwa mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao utajadili kwa uwazi na udhati maswala muhimu yanayoathiri dunia hasa nchi zinazoendelea.

    Mtafiti wa maswala ya maendeleo wa Chuo Kikuu cha Afrika Kusini Bw Sabelo Gatsheni Ndlovu amesema mkutano huo hauwezi kupuuza changamoto za mazingira, ugaidi na maendeleo, hasa katika wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na ongezeko dhaifu la uchumi na inahitaji kupata suluhisho.

    Bw Ndlovu pia amezitaka nchi za magharibi ziache kulaumu wengine kwenye suala la mabadiliko ya hali ya hewa, na badala yake kuchukua hatua madhubuti. Pia amezilaani nchi za magharibi kwa kuchochea migogoro kwenye baadhi ya nchi za Afrika na Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako