• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Conseslus Kipruto avunja rikodi ya Olimpiki ya mita 3000 kuruka viunzi

    (GMT+08:00) 2016-08-18 09:26:19

    Jana mchana Wakenya walijumuika pamoja kumshangilia mwanariadha aliyeshiriki kwenye mbio za kuruka viunzi mita 3000, Conseslus Kipruto baada ya kuimarisha nguvu ya Kenya na kuvunja rikodi ya zamani ya Olimpiki ya dakika 8 sekunde 5 na nukta 51 ambayo iliwekwa na Julius Kariuki mwaka 1988 kwenye Olimpiki ya Seoul na sasa ameandika muda wa dakika 8 sekunde 3 na nukta 29. Baada ya kuongoza kwa kwa muda mrefu kwenye mbio hizo Mmarekani Evan Jager alitupwa nafasi ya pili kwenye mzunguko wa mwisho na kuondoka na medali ya fedha baada ya kuwa na muda wa dk 8:04.28, nafasi ya tatu ilitwaliwa na bingwa mtetezi Mkenya Ezekiel Kemboi aliyekimbia kwa muda wa Dakika 8:08.47 lakini baadaye aliambiwa hastahili nafasi hiyo baada ya kukiuka sheria zikiwemo kukanyaga ndani ukingo hivyo medali ya shaba ikaenda Ufaransa kwa Mekhissi Mahiedine .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako