• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatarajia mkutano wa kilele wa G20 wa Hangzhou utachangia ongezeko la biashara duniani

    (GMT+08:00) 2016-08-18 19:37:07

    Naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani WTO Bw. Yi Xiaozhun amesema mkutano wa kilele wa G20 utachangia ongezeko la biashara duniani kama wakuu wa nchi hizo watajadiliana kiujenzi kuhusu biashara na uwekezaji, na kuamua kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa biashara wa kundi la nchi 20.

    Bw. Yi amesema hayo kabla ya mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika mapema mwezi ujao mjini Hangzhou, mashariki mwa China. Amesema nchi mbalimbali zinatumia njia zote kukuza uchumi wao, lakini bado zipo nguvu na nafasi nyingi kwao kufanya ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji. Ameipongeza China ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa G20 wa safari hii kwa kupendekeza kufanya ajenda zinazohusiana na biashara na uwekezaji ziwe na hadhi sawa na ile ya sera za kifedha kwa ajili ya kujadiliwa, na kusema huu ni uamuzi sahihi na muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako