• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya huduma ya Taxi ya China Didi yachaguliwa kwenye orodha ya "Kubadilisha Dunia" ya gazeti la fortune

    (GMT+08:00) 2016-08-23 19:03:04

    Kampuni ya huduma ya taxi ya China Didi Chuxing imechaguliwa kuingia kwenye orodha ya makampuni makubwa yanayoleta mabadiliko duniani mwaka 2016 kwenye gazeti la Fortune, muda mfupi baada ya kununua huduma ya taxi ya Uber.

    Kampuni ya Didi imetajwa kuwa katika nafasi ya 30 ikiwa na thamani ya dola bilioni 35, imepata nafasi hiyo hasa kutokana na mchango wake kwenye kulinda mazingira.

    Kampuni ya dawa ya Uingereza GlaxoSmithkline ndiyo inaongoza, ikifuatiwa na kampuni ya Israel ya kuondoa chumvi kwenye maji, na kampuni ya General Electric ya Marekani.

    Mwaka jana kampuni ya Didi ilisaidia kupunguza safari milioni moja za magari kwa siku, na kuokoa lita milioni 500 za mafuta, na kupunguza tani milioni 13.5 hewa chafu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako