• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Unajua mdomo wa mbu si sindano 1 bali ni sindano 6?

    (GMT+08:00) 2016-08-24 14:20:31

    Unafikiri mbu jike anachoma sindano kwenye mshipa wa damu, na kuingiza kemikali mbaya zinazosababisha ngozi yako kuwasha halafu kuvuta damu yako? Lakini ukweli si rahisi kama unavyofikiri.

    Mdomo wa mbu unaouona moja kwa moja ni mdomo wa chini. Unafanya kazi kama ala ya upanga. Ndani yake kuna "sindano" sita, ambazo ni pamoja na mdomo wa juu, taya mbili za juu, taya mbili za chini na ulimi. Wakati mbu anapochoma ngozi yako, mdomo wa chini unapinda, na "sindano" zinazohifadhiwa ndani yake zitatolewa. Lakini sehemu ya mbele ya mdomo wa chini utawekwa juu ya ngozi ili kuongoza "sindano" kuingia ngozini kama unavyoshika msumari kwa mkono mmoja unapopiga msumari kwa mkono mwingine.

    taya za juu na chini ni vifaa muhimu vya kuchoma ngozi. taya hizo si kama tu ni kali sana, bali pia ni laini. Mbu hana uwezo wa kugundua mahali pa mshipa wa damu bila kutafuta, hivyo taya hizo laini zinaweza kupinda chini ya ngozi kwa urahisi ili kutafuta mshipa wa damu.

    Baada ya kugundua mshipa wa damu, mdomo wa juu na ulimi utaanza kufanya kazi. Ulimi unatumiwa kuingiza mate ndani ya ngozi ya binadamu. Mate ya mbu yana kemikali za kuzuia damu zisigande na kutia ganzi ili mbu asigunduliwe na binadamu. Lakini kama mbu huyu ana vijidudu vya malaria au virusi vya Zika mwilini mwake, vijidudu na virusi hivi vitaingia mwilini mwa binadamu kupitia mate yake. Mwishowe mdomo wa juu unafanya kazi ya kuvuta damu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako