• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imejiandaa vizuri kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2016-08-25 09:57:14

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang jana amesema, China imefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika mjini Hangzhou.

    Bw. Lu Kang amesema chini ya juhudi za pande mbalimbali, mkutano huo unatarajiwa kufikia makubaliano karibu 30. Ameongeza kuwa, sauti za pande mbalimbali zitasikika kwenye mkutano huo unaozishirikisha nchi za G77, nchi za Afrika, nchi zilizonyuma zaidi kimaendeleo, nchi za visiwa, nchi za jumuiya ya madola na zile zinazozungumza Kifaransa.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Japan jana baada ya kukutana na mwenzake wa Japan Kisida Fumio amesema, Japan ni nchi mwanachama muhimu wa G20, China inamkaribisha waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kuja China kuhudhuria mkutano wa G20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako