• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ulaya inatarajia mkutano wa G20 utakamilisha usimamizi wa fedha duniani

    (GMT+08:00) 2016-08-28 15:50:21
    Wanasiasa na wasomi wengi kutoka Ulaya wamesema, China imepata mafanikio katika kuhimiza G20 kukamilisha usimamizi wa fedha mwaka huu, na wameeleza matarajio yao kuwa mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika tarehe 4 hadi tarehe 5 mwezi ujao mjini Hangzhou, China, utahimiza zaidi mageuzi ya mfumo wa fedha duniani, ili kuchangia ukuaji wa uchumi duniani.

    Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mambo ya uchumi ya Bruegel Guntram Wolff anasema ajenda kuhusu usimamizi wa fedha itakayojadiliwa kwenye mkutano wa G20 wa safari hii ina umuhimu mkubwa kwa Ulaya, ambapo baadhi ya nchi zao zinakumbwa na hatari ya kuongezeka kwa msukosuko wa sekta ya benki, njia bora za usimamizi wa fedha zinahitajika .

    Naye mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya uchumi na fedha Pierre Moscovici amesema, China siku zote inafanya juhudi kuharakisha mageuzi ya uchumi na fedha duniani, hususan kuongeza uwakilishi na haki za kutoa maoni za makundi ya kiuchumi yaliyojitokeza upya na nchi zinazoendelea, na Umoja wa Ulaya unakaribisha China kufanya kazi kubwa katika kuimarisha utulivu na maendeleo ya uchumi duniani.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako