• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maafisa wa Olimpiki Kenya waachiliwa kwa dhamana

    (GMT+08:00) 2016-08-30 09:12:54
    Mahakama nchini kenya imewaachilia kwa dhamana maafisa wawili wa kamati ya kitaifa ya Olimpiki wanaochunguzwa kwa usimamizi mbaya wa kikosi cha kenya kilichoshiriki mashindano ya olimpiki mjini Rio.

    Katibu mkuu wa kamati ya kitaifa ya olimpiki nchini Kenya (Nock) Francis Paul na Pius Ochieng ambaye ni naibu mwenyekiti wa Nock waliachiliwa kwa dhamana ya dola 2000.

    Hata hivyo jaji aliwaamrisha wasiende ofisi zao, kutozungumza na mashahidi na kuwaamrisha kusalimisha paspoti zao.

    Wakuu wa mashtaka walikuwa wametaka wawili hao kuzuiwa rumande kwa siku 21 wakati wanapowachunguza kwa mashtaka ya wizi, matumizi mabaya ya ofisi zao na kutelekeza majukumu yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako