• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchango wa China kwa kundi la G20 utachangia ongezeko la uwekezaji duniani

    (GMT+08:00) 2016-08-31 19:46:46

    Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa G20 kufanyika Hangzhou, mashariki mwa China, katibu mkuu wa zamani wa kamati ya kanda ya Ulaya na mtaalamu wa masuala ya China kwenye Taasisi ya Ulaya Gerhard Stahl amesema kuimarisha uratibu kati ya nchi mbalimbali kuhusu sera za uchumi, kuchukua tahadhari na vitendo vya kujilinda kibiashara na kujenga soko lililo wazi yatakuwa majukumu muhimu ya kundi la G20. Pili Mwinyi anatuelezea zaidi.

    Mkutano wa G20 unaolenga kuongeza ushirikiano wa uchumi wa dunia umetoa nafasi muhimu ya mawasiliano kwa nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea, na biashara ya kimataifa isiyo na nguvu, kuibuka kwa vitendo vya kujilinda kibiashara ni changamoto zinazolikabili kundi la G20. Bw. Stahl anasema,

    "Naona G20 inapaswa kubeba jukumu muhimu, na kuhimiza uratibu kati ya makundi makubwa ya kiuchumi duniani katika utekelezaji wa sera za uchumi, kama vile China, Asia, Ulaya na Marekani, na hata nchi zinazoendelea za Afrika. Mkutano wa kilele wa G20 unatakiwa kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia."

    Bw. Stahl anaona kuwa China ikiwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa G20 wa safari hii imehimiza ongezeko la uwekezaji kupitia kutoa mapendekezo yake mbalimbali.

    "China inashika nafasi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi, na kuwa na umuhimu mkubwa kwa biashara na uwekezaji duniani. Mapendekezo yaliyotolewa na China ya kujenga Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB na "Ukanda Mmoja na Njia Moja" yameboresha mazingira ya uwekezaji sio tu nchini China, bali pia kwenye bara la Asia na Ulaya. Naona China inaweza kuchangia ushirikiano wa kimataifa chini ya utaratibu wa kundi la G20 kutokana na nguvu zake za fedha na malengo ya kimkakati, na kusaidia kuongeza ukubwa wa uwekezaji duniani."

    Kabla ya hapo, mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za kundi la G20 ulitoa taarifa ukisema kujitoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya kumeongeza hali ya uhakika kwa uchumi wa dunia, na nchi wanachama mbalimbali zimejiandaa vizuri kukabiliana na changamoto hizo. Akizungumzia kuhusu Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya kama kutaathiri vibaya ushirikiano wa kundi la G20 katika siku za baadaye, profesa Stahl anasema,

    "Kwa ujumla, naona kujitoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya hakutaleta tishio kubwa kwa uchumi, kwani kabla ya kupigwa kura za maoni, Uingereza ilikuwa na uhusiano wa aina tofauti na nchi za Umoja wa Ulaya. Hivyo kwangu mimi nina matumaini makubwa na kuona kuwa Uingereza inaweza kupata njia ya ushirikiano wa karibu na Umoja wa Ulaya kupitia mashauriano, na kuendelea kuwepo ndani ya soko la Ulaya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako