• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mambo ya fedha yasiyochafua mazingira yataorodheshwa kuwa ajenda ya mkutano wa G20 kwa mara ya kwanza

    (GMT+08:00) 2016-09-02 15:14:56
    Naibu mkuu wa Benki Kuu ya China Bw. Yi Gang leo mjini Hangzhou amesema, kikundi kipya cha utafiti wa mambo ya fedha yasiyochafua mazingira kimeanzishwa, na ajenda kuhusu mambo hayo itajadiliwa kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa kilele wa kundi la G20 utakaoanza kesho mjini Hangzhou, China.

    Bw. Yi amesema, ripoti ya jumla kuhusu mambo ya fedha yasiyochafua mazingira ya mkutano wa G20 imeshaandaliwa, ambayo inaweka wazi maana na malengo ya mambo ya fedha yasiyochafua pamoja na changamoto zilizopo. Ripoti hiyo itasaidia kutoa ushauri kwa nchi mbalimbali kukuza mambo hayo na kuunga mkono uchumi wa dunia kuelekee kuwa ule usiochafua mazingira.

    Inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2020 fedha zitakazohitajika kuwekeza kwenye sekta ya nishati zisizochafua mazingira zitafikia dola za kimarekani bilioni 500, na kuanzisha mfumo wa mambo ya fedha yasiyochafua mazingira kutatoa fursa mpya kwa sekta za viwanda na biashara duniani.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako