• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa ushirikiano katika kupunguza uzalishaji wa kupita kiasi

    (GMT+08:00) 2016-09-02 20:36:09

    Naibu waziri wa fedha wa China Bw. Zhu Guangyao amesema uzalishaji wa kupita kiasi umekuwa suala linaloikabili dunia nzima, na linatakiwa kushughulikiwa kwa juhudi za pamoja, na China inatarajia kuwa jumuiya ya kimataifa inaweza kuwa na mtazamo huu na kutoa ushirikiano badala ya kutupa lawama.

    Bw. Zhu amesema, China ni nchi iliyotangulia duniani kwa kuchukua hatua ya kupunguza uzalishaji wa kupita kiasi, na inayaunga mkono makampuni ya mafuta na makaa ya mawe kuungana kwa kufuata mahitaji ya soko na kuanzisha mahakama ya kushughulikia kesi za kufilisika kwa makampuni. Ameongeza kuwa, kusukuma mbele mageuzi kwenye sekta ya utoaji wa bidhaa na kuongeza ubora wa bidhaa ni kazi muhimu katika kutekeleza mageuzi ya uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako