• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China afafanua ufumbuzi wa kichina kwenye ufunguzi wa mkutano wa kilele wa G20

    (GMT+08:00) 2016-09-03 19:22:44

    Mkutano wa kilele wa viwanda na biashara wa kundi la nchi 20 B20 umefunguliwa leo alasiri mjini Hangzhou, China. Rais Xi jinping wa China amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo, akifafanua kwa kina maoni na mapendekezo yake kuhusu uchumi wa China na wa dunia, na usimamizi wa uchumi wa dunia.

    Mkutano wa B20 ukiwa ni sehemu muhimu ya mkutano wa kilele wa G20 umefunguliwa leo mjini Hangzhou. Katika hali ambayo ufufukaji wa uchumi wa dunia ni dhaifu, mwelekeo wa uchumi wa China unafuatiliwa sana duniani. Akihutubia ufunguzi wa mkutano wa B20, rais Xi Jinping wa China amejibu ufuatiliaji wa dunia kwa China.

    "Watu wengi wanafuatilia kama uchumi wa China unaweza kudumisha ukuaji endelevu, kama China itaendelea kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango, na kama China inaweza au la kuepuka "kikwazo cha mapato ya kati" yaani Middle Income Trap. Vitendo huwa ni muhimu zaidi kuliko maneno. China imejibu kivitendo maswali haya. Mwanzoni mwa mwaka huu, China imetoa mwongozo wa mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano, ambao unalenga kutatua masuala makubwa yakiwemo kutokuwa na uwiano na uratibu katika maendeleo, na maendeleo yasiyo endelevu, na unasisitiza umuhimu na ulazima wa kujenga na kutekeleza wazo la maendeleo yenye uvumbuzi, uwiano, kutochafua mazingira, kufungua mlango na kunufaisha wote. China ya leo iko kwenye mstari wa mwanzo mpya wa kihistoria."

    Rais Xi amefafanua zaidi kuwa mwanzo huo mpya ndio ni mwanzo mpya kwa China kuimarisha mageuzi na kuongeza msukumo mpya wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ni mwanzo mpya kwa China kuzoea hali mpya ya kawaida ya maendeleo ya uchumi, na kugeuza njia za kujiendeleza kiuchumi, na pia ni mwanzo mpya kwa China kuimarisha maingiliano ya kina na dunia na kufungua mlango zaidi kwa nje.

    Hivi sasa uchumi wa dunia unaendelea kudidimia, huku kasi ya ongezeko la biashara ya kimataifa ikifikia kiwango cha chini zaidi katika miaka 30 iliyopita. Wakati huohuo, changamoto za kisiasa na kiusalama duniani pamoja na masuala mbalimbali ya kikanda, vimetatanisha zaidi uchumi wa dunia. Katika hali hiyo, jumuiya ya kimataifa imekuwa na matarajio makubwa kwa China. Kwenye hotuba yake, rais Xi Jinping wa China ametoa ufumbuzi wa kichina kwa uchumi wa dunia unaokabiliwa na matatizo.

    "China inatumai kushirikiana na pande mbalimbali, na kusukuma mbele mkutano wa kilele wa G20 wa Hangzhou uweze kutoa ufumbuzi jumuishi wa kutatua kabisa matatizo yaliyopo, ili kuelekeza uchumi wa dunia kwenye njia sahihi ya ukuaji imara na endelevu wenye uwiano na ushirikishi. Kwanza ni kujenga uchumi wa dunia unaohimiza uvumbuzi na kutafuta msukumo mpya wa ukuaji. Pili ni kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, na kupanua mustakbali wa maendeleo. Tatu ni kujenga uchumi wa dunia unaoungana, ili kuchochea maingiliano na ushirikiano. Nne ni kujenga uchumi wa dunia lenye ushirikishi, ili kuimarisha msingi wa kunufaishana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako