• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Marekani, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wahudhuria hafla ya kukabidhi hati idhini za makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2016-09-03 20:14:56

    Rais Xi Jinping wa China, rais Barack Obama wa Marekani na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon wamehudhuria kwa pamoja hafla ya kukabidhi hati idhini za makubaliano ya Paris mjini Hangzhou, China mapema leo.

    Rais Xi amesema, mabadiliko ya hali ya hewa yanahusiana na maslahi ya wananchi na mustakbali wa binadamu. China imetoa mchango muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, imependekezo kundi la G20 kutoa taarifa ya mwenyekiti kuhusu suala la hali ya hewa na kusaini mapema makubaliano ya Paris. Rais Xi amesisitiza kuwa China ikiwa ni nchi ya kuwajibika na mshiriki muhimu wa usimamizi wa hali ya hewa duniani, itatekeleza wazo la maendeleo yenye uvumbuzi, uwiano, kutochafua mazingira, kufungua mlango na kunufaisha wote, kuendelea na juhudi za kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa hewa chafu, ili kuingia kwenye enzi mpya ya ustaarabu wa kiikolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako