• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa B20 wafunguliwa China

  (GMT+08:00) 2016-09-03 21:07:44

  Mkutano wa kilele wa viwanda na biashara wa kundi la G20 wa mwaka 2016, ambao unajulikana kama B20, umefunguliwa leo alasiri mjini Hangzhou, China. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo.

  Mkutano wa kilele wa B20 ukiwa ni sehemu muhimu ya mkutano wa kilele wa Kundi la G20 utakaofanyika mjini Hangzhou, unaweka jukwaa muhimu kwa sekta za viwanda na biashara za kimataifa kushiriki kwenye usimamizi wa uchumi wa dunia na utungaji wa kanuni za uchumi na biashara za kimataifa.

  Wajumbe zaidi ya 800 kutoka nchi na sehemu 32 na mashirika 26 ya kimataifa wamehudhuria mkutano huo, ambao utawasilisha ripoti ya mapendekezo ya kisera ya B20 ya mwaka 2016 kwenye mkutano wa kilele wa G20.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako