• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano usio rasmi wa viongozi wa nchi za BRICS wafanyika huko Hangzhou, China

    (GMT+08:00) 2016-09-04 15:54:14
    Mkutano usio rasmi wa viongozi wa nchi za BRICS umefanyika leo asubuhi huko Hangzhou, China, na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping wa China, waziri mkuu wa India Narendra Modi, rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, rais Michel Temer wa Brazil na rais Vladimir Putin wa Russia.
    Akihutubia mkutano huo, rais Xi kwanza amempongeza rais Temer wa Brazil kwa kujiunga na familia ya ushirikiano ya nchi za BRICS. Pia amesema, BRICS ni kundi linaloongoza nchi zinazojitokeza kiuchumi na nchi zinazoendelea, ambazo pia ni nchi wanachama muhimu wa kundi la G20. Nchi wanachama wa BRICS wanatakiwa kufuata mkondo wa historia, kushikilia mwelekeo mkuu wa kimataifa, kuimarisha uratibu na ushirikiano, na kuchukua nafasi muhimu katika usimamizi wa kimataifa.
    Rais Xi pia amesema, tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kutokana na juhudi za pamoja na nchi tano za BRICS na msukumo wa nchi mwenyekiti India, ushirikiano kati ya nchi za BRICS umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, huku sekta za ushirikiano zikipanuliwa na mafanikio mengi zaidi yakipatikana.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako