• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa G20 wafikia makubaliano kuhusu mapambano na ugaidi na suala la wakimbizi

    (GMT+08:00) 2016-09-05 09:52:24

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bi Hua Chunying amesema, mawaziri wa mambo ya nje wa G20 wamefikia makubaliano kuhusu masuala mengi yakiwemo mapambano dhidi ya ugaidi, suala la wakimbizi, mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo endelevu.

    Msemaji huyo amesema, katika mkutano usio rasmi uliowakutanisha mawaziri hao kando ya mkutano wa wakuu wa G20, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kushirikiana kuanzisha uhusiano wa kimataifa wa aina mpya unaolenga kutafuta ushirikiano wa kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako