• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa viwanda na biashara wa G20 wapata mafanikio makubwa

  (GMT+08:00) 2016-09-05 10:32:39

  Mkutano wa kilele wa viwanda na biashara wa kundi la nchi 20 G20 wa mwaka 2016 umemalizika kwa mafanikio huko Hangzhou, China.

  Mkutano huo ulimalizika jana ambapo ulitoa mapendekezo 20 ya utungaji wa sera na hatua 76 za kuhimiza uvumbuzi, kuongeza biashara ya kimataifa na kuhimiza maendeleo shirikishi. Mapendekezo hayo ni pamoja na kujenga soko la kukusanya fedha kwa ajili ya maendeleo ya kijani, kujenga jukwaa la biashara duniani kupitia Internet, na kuziunga mkono kampuni ndogo na za ukubwa wa kati.

  Washiriki wa mkutano huo akiwemo rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, wamesisitiza haja ya kubadili njia ya maendeleo kwa kufanya uvumbuzi wakati uchumi wa dunia unakosa uwiano na kukabiliwa na hatari ya kudidimia zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako