• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuongezeka kwa joto baharini huenda kukasababisha samaki wawe na sumu

    (GMT+08:00) 2016-09-09 10:14:40

    Shirika la uhifadhi wa mazingira la kimataifa limetoa ripoti likisema kuongezeka kwa joto baharini ni changamoto kubwa zaidi kwa mazingira ya viumbe kote duniani.

    Tokea miaka ya 70 karne iliyopita, shughuli za binadamu zimesababisha kuongezeka kwa joto duniani, na asilimia 93 ya joto lilifyonzwa na bahari.

    Kuongezeka kwa joto baharini kumewalazimisha wadudu wadogowadogo wanaoishi majini, yavuyavu, kobe na ndege kuhama maeneo yanayokaribia ncha za dunia, na kusababisha kupungua kwa maeneo ya kuzaliana na kiwango cha uzazi.

    Kuongezeka kwa joto baharini pia kutaharibu makazi ya samaki na kuwalazimisha kuhamia mahali baridi zaidi. Inakadiriwa kuwa uzalishaji wa samaki katika ukanda wa tropiki utapungua katika miongo kadhaa ijayo.

    Kuongezeka kwa joto baharini pia kutaongeza maambukizi ya magonjwa mbalimbali, ikiwemo kipindupindu, kwani vijidudu vinapenda zaidi kuishi katika maji ya uvuguuvugu. Aidha, mwani wenye sumu aina ya CTX utakua kwa wingi zaidi, samaki wakila mwani huo, sumu itahifadhiwa kwenye nyama zao, na watu wakila samaki hao wataumwa vibaya. Sumu ya CTX ni kali zaidi kuliko sumu ya TTX (sumu ya bunju) kwa mara 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako