• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwanini panda wamewekwa kwenye orodha ya wanyama walioko katika hali ngumu badala ya walioko hatarini?

    (GMT+08:00) 2016-09-18 09:54:10

    Shirika la uhifadhi wa mazingira ya kimaumbile duniani IUCN limewaweka panda kwenye orodha ya viumbe vilivyoko katika hali ngumu. Lakini kabla ya hapo, panda wako kwenye orodha ya viumbe vilivyoko hatarini. Je, kwanini shirika hili limefanya mabadiliko hayo?

    Zamani idadi ya panda ilikuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa, na makundi ya panda yaligawanyika katika vikundi vidogo vidogo, hivyo walikuwa hatarini. Uchunguzi mpya unaonesha kuwa hali hiyo inabadilika, idadi ya panda inaongezeka, makundi ya panda yamekuwa makubwa zaidi, na makazi yao yamerudishwa hatua kwa hatua. Uchunguzi uliofanyika mwaka 2004 ulikadiria kuwa kuna panda 1,596 nchini China, na sasa idadi hiyo huenda ikawa imefikia 1864.

    Ingawa hali ya panda inaonesha mwelekeo mzuri, lakini bado wanakabiliwa na tishio jipya. Hatua za sasa za kuwahifadhi panda zikifutwa, watakuwa hatarini tena. Wakati joto la dunia linapoendelea kuongezeka, inakadiriwa kuwa maeneo yenye mianzi ambayo ni chakula kikuu cha panda yatapungua, na kusababisha idadi ya panda kupungua tena, na baadhi ya makundi yatakabiliwa na tishio kubwa zaidi.

    China itaendelea kuchukua hatua kuunganisha makazi ya panda yaliyogawanyika kutokana na vitendo vya binadamu, ili kuwasaidia panda kutoka makundi mbalimbali kuwasiliana na kuzaliana, pia itajitahidi kupunguza athari mbaya ya kuongezeka kwa joto duniani, na kudhibiti matishio mengine mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako