• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaadhimisha kumbukumbu ya Tukio la Septemba 18

    (GMT+08:00) 2016-09-18 20:23:22

    Naibu waziri mkuu wa China Bi. Liu Yandong amegonga kengele ya kumbukumbu ya miaka 85 ya Tukio la Septemba 18 mjini Shenyang, mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China.

    Mbele ya maofisa wa serikali na wawakilishi wa wananchi, Liu aligonga kengele mara 14, ikiwa ni ishara ya miaka 14 ambayo wananchi wa China walipambana na wavamizi wa Japan. Akizungumza baada ya hafla hiyo, Bi. Liu amesema kuwa taifa la China ni taifa linalopenda amani na lina nia thabiti ya kulinda amani. Amesema Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa China wanaelewa thamani ya amani na maendeleo, na wanachukulia kama jukumu lao kuboresha amani ya dunia na maendeleo.

    Septemba 18 mwaka 1931, vikosi vya Japan vililipua sehemu ya reli iliyokuwa inaidhibiti karibu na mji wa Shenyang, kisha kuwatuhumu askari wa China kwa hujuma, kwa lengo la kufanya shambulizi. Siku hiyo hiyo, askari wa Japan walishambulia kwa mabomu kambi za jeshi karibu na mji huo, na huo ukawa ni mwanzo wa uvamizi wa Japan nchini China uliodumu kwa miaka 14.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako