• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sokwe watu wenye tabia ya kushindana wamejifunza kushirikiana ili kupata chakula

  (GMT+08:00) 2016-09-19 09:08:04

  Tofauti na binadamu, sokwe watu ni wanyama wanaopenda zaidi kushindana badala ya kushirikiana. Lakini Dr. Malini Suchak na wenzake kutoka kituo cha utafiti wa jamii ya nyani cha kitaifa cha Yerkes, Marekani wamegundua kuwa sokwe watu pia wanaweza kushirikiana kwa karibu.

  Watafiti hao wamefanya majaribio kuhusu sokwe watu 11 walioishi pamoja kwa zaidi ya miaka 20. Sokwe wawili au watatu wakivuta kifaa kwa pamoja, watapata chakula. Sokwe hao hawajafundishwa na watu kuhusu njia ya kupata chakula, wanatakiwa kufikiri na kujaribu wao wenyewe.

  Watafiti walifanya majaribio kwa saa 94, wakagundua kuwa ingawa sokwe walifanya ushindani kwa zaidi ya mara 600, lakini pia wamefanikiwa kushirikiana kwa mara 3656.

  Katika majaribio hayo, mwanzoni sokwe hao walipojifunza kuvuta kifaa walishirikiana vizuri, lakini baada ya sokwe wengi zaidi kujua namna ya kuvuta kifaa, walianza kushindana na hata kupora chakula cha wengine. Baada ya sokwe hao kufanya hivyo kwa muda kadhaa, waligundua kuwa wenzao watakasirika, hivyo wakawaacha na kushirikiana na wengine, mwishowe walitambua kuwa kushirikiana ni uamuzi mzuri zaidi kuliko kushindana, na wakashirikiana tena na kwa karibu zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako