• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utatuzi wa suala la wakimbizi wahitaji juhudi za pamoja za kurejesha amani na kufufua uchumi

    (GMT+08:00) 2016-09-20 18:17:35

    Wakati msukosuko wa wakimbizi unaotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria na mapambano nchini Iraq na Afghanistan unapoendelea, nchi mbalimbali duniani zinatakiwa kufahamu kuwa juhudi za pamoja zinazolenga vyanzo vya asili badala ya maneno matupu ni njia pekee ya kutatua suala hilo. Guo Cong ana maelezo zaidi:

    Katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu msukosuko wa wakimbizi uliofanyika huko New York, viongozi wa dunia wamepitisha azimio linalolenga kushughulikia uhamiaji wa wakimbizi zaidi ya milioni 20 kote duniani kwa njia ya ushirikiano na yenye huruma zaidi.

    Ni wazi kuwa, nchi za magharibi haswa Marekani ambayo inawajibika kwa kiasi kikubwa na vita na mapambano yaliyotokea katika sehemu hizo, zinatakiwa kuongoza katika utatuzi wa mgogoro wa wakimbizi, kwa sababu mambo waliyoyafanya kwenye sehemu hizo kwa kiasi fulani yalisababisha vita, vurugu na umaskini, ambazo ni vyanzo vya mgogoro wa wakimbizi.

    Katika miaka 6 iliyopita, vita vimesababisha wakimbizi zaidi ya milioni 4.8 walioandikishwa nchini Syria, ambao walilazimishwa kukimbia makwao na kwenda nchi na sehemu za jirani, haswa Ulaya. Vita hivyo vinaonekana kuendelea baada ya usimamishaji vita uliofikiwa na kudumu kwa wiki moja chini ya upatanishi wa Russia na Marekani nchini Syria kumalizika Jumatatu.

    Wakati huohuo, hatua za kisiasa zinazochukuliwa na nchi tajiri za Ulaya zinaweza kuathiri vibaya nchi nyingine za kanda hiyo. Kwa mujibu wa Jopo la Washauri la Taasisi ya Maendeleo ya Nje ya Uingereza, hatua za nchi tajiri kudhibiti idadi ya wakimbizi zimechochea sera zinazofanana kutekelezwa katika sehemu ambazo kwa asili zinapokea wakimbizi wengi.

    Taasisi hiyo imetoa mifano ya Jordan ambayo imekataa kupokea wakimbizi elfu 70 kutoka Syria waliokwama jangwani, na mpango wa Kenya wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab na kurejesha idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Somalia nchini mwao.

    Kuondoa mizizi ya mgogoro wa Syria kwa kumaliza vita, kurejesha utulivu wa jamii na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi, kuongeza nafasi za ajira na elimu ni njia ya msingi ya kusaidia wakimbizi kurudi nyumbani.

    Hivi leo, kwa kuwa hakuna nchi hata moja inayoweza kukwepa athari za suala la kimataifa la wakimbizi na wahamiaji, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua za haraka na zenye nguvu kwa pamoja ili kukabiliana na suala hilo kwa ufanisi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako