• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guardiola asema Yaya Toure hawezi kuichezea Man City hadi wakala wake aombe radhi

    (GMT+08:00) 2016-09-21 09:31:34

    Jana kocha wa Man City ya England Pep Guardiola aliweka wazi kwa nini hamchezeshi kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure. Akiongea na waandishi wa habari Guardiola alisema, Yaya Toure hawezi kuichezea tena Man City hadi atakapoomba radhi kwa wachezaji wenzake na timu kwa ujumla, kutokana na maneno yaliyotolewa na wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk ambaye anamponda Guardiola kuwa amemdhalilisha Toure kwa kumuacha katika kikosi cha UEFA.

    Toure ambaye ametangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya Ivory Coast, ameshinda matajia 113 akiwa na timu yake ya taifa toka alipoanza kuichezea 2004 na ameshinda taji la mataifa ya Afrika 2015, ila Pep Guardiola anatajwa kutomuhitaji kiungo huyo kwani toka 2010 alisababisha nyota huyo akahama FC Barcelona na kujiunga na Man City.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako