• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Konokono anafanya uamuzi kwa seli mbili za ubongo

  (GMT+08:00) 2016-09-21 14:35:08

  Watafiti wamegundua kuwa konokono anaweza kufanya uamuzi kwa ubongo wake wenye seli mbili tu, ambazo moja inamwambia kama ana njaa au la, na nyingine inamwambia kama kuna chakula au la. Ugunduzi huo utawasaidia wahandisi kutengeneza roboti inayofanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

  Prof. George Kemenes wa Chuo Kikuu cha Sussex alisema tunapofanya vitendo mbalimbali hatujui jambo gani linatokea ndani ya ubongo wetu. Seli mbili za neva za konokono zinaonesha kuwa zinaweza kutimiza mambo mbalimbali kwa ufanisi mkubwa.

  Watafiti wamepima mabadiliko ya seli za neva za ubongo wa konokono wanaotafuta mboga kwa elektrodi, na kugundua kuwa seli moja inafanya kazi ya kudhibiti na nyingine inafanya kazi ya kuhimiza, zinaitikiana na kumsaidia konokono kufanya uamuzi.

  Kutafuta chakula ni kitendo chenye lengo la wazi. Wanyama wanapotafuta chakula, wanatakiwa kuchambua mazingira na hali yake na kubana matumizi ya nishati kadri awezavyo ili kufanya uamuzi mzuri zaidi.

  Watafiti wamesema ugunduzi wao utawasaidia wanasayansi kutafiti mifumo ya neva ya wanyama wengine, na kuwasaidia wahandisi kusanifu ubongo wa roboti zinazoweza kufanya kazi ngumu kwa vipuri vichache zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako