• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakaribisha nchi nyingi zaidi kujiunga na Makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2016-09-22 21:02:30

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Lu Kang leo amesema, China inazikaribisha nchi nyingi zaidi kushiriki kwenye makubaliano ya Paris, ili kuwezesha utekelezaji wake mapema. Lu amesema suala la mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto inayoikabili dunia nzima, na inahitaji ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa. Ameongeza kuwa, China inajitahidi kushiriki kwenye mchakato wa pande nyingi katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Wakati huohuo, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon jana amesema kwamba hadi sasa nchi 60 zimekabidhi hati idhini za Makubaliano ya Paris, ambayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako