• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashine za uchapishaji wa 3D zinaweza kuchapisha vyakula gani?

    (GMT+08:00) 2016-09-23 10:27:36

    Tukizungumzia mashine ya kuchapisha vyakula, kwanza tunahitaji kutaja teknolojia ya uchapishaji wa 3D.

    Mwaka 1986 Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Marekani kilivumbua mashine ya kwanza ya uchapishaji wa 3D, baadaye teknolojia hii ilipata maendeleo ya kasi na kutumiwa katika kazi mbalimbali.

    Mwaka 2011, watafiti wa Uingereza walisanifu mashine ya kwanza ya kuchapisha chokoleti. Baadaye kampuni ya Hispania iliboresha teknolojia yao na kutengeneza mashine ya kuchapisha chakula iitwayo Foodini.

    Siku hizi mashine za uchapishaji wa 3D zinaweza kuchapisha zaidi ya aina 30 ya vyakula, vikiwemo chokoleti, pipi, jeli, biskuti, keki, chipsi, jamu za matunda au mboga, vyakula vyenye nyama, jibini na mtindi. Mashine ya kwanza ya uchapishaji wa 3D wa vyakula ni ya kuchapisha chokoleti, na pia ni mashine inayopata maendeleo ya kasi zaidi.

    Teknolojia ya kuchapisha vyakula inasaidia kutoa vyakula tofauti kwa mujibu wa watu mbalimbali wakiwemo watoto na wazee. Kampuni moja ya Ujerumani imezalisha chakula kiitwacho "Smooth food" ambacho ni rahisi kutafunwa na kumezwa. Chakula hiki huenda kitatumiwa kwa wingi katika kazi ya kuwatunza wazee.

    Aidha, teknolojia hii inawawezesha watu kuchapisha vyakula vipya kwa kutumia lishe za mwani, majani ya viazi sukari na wadudu, ili kutatua tatizo la ukosefu wa chakula duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako