• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Canada

    (GMT+08:00) 2016-09-23 20:18:39

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alifanya mazungumzo na mwenzake wa Canada Bw. Justin Trudeau huko Ottawa.

    Katika mazungumzo yao, Bw. Li amesema, China inapenda kuimarisha mawasiliano na Canada na kuzidisha uaminifu wa kisiasa, ili kuwanufaisha watu wa nchi zote mbili. Ameongeza kuwa China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na Canada, na kupanua masoko ya upande wa tatu kwa pamoja.

    Kwa upande wake, Trudeau amesema, kuanzishwa kwa utaratibu wa mazungumzo kati ya mawaziri wakuu wa Canada na China kila mwaka, kuna umuhimu mkubwa katika kukuza uhusiano na kupanua ushirikiano kati ya nchi zote mbili. Amesema, Canada inapenda kuimarisha uratibu na ushirikiano na China katika sekta mbalimbali, na kukabiliana na changamoto za dunia kwa pamoja.

    Wakati huo huo, Bw. Li Keqiang amekutana na spika wa baraza la juu la bunge la Canada George Furey na spika wa baraza la chini la bunge hilo Geoff Regan. Li amesema kwamba Bunge la Umma la China linapenda kubadilishana mawazo na mabaraza hayo mawili ya Canada, na kutoa mchango kwa ajili ya kuzidisha uelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako