• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Siafu wanajuaje njia ya kurudi nyumbani?

  (GMT+08:00) 2016-09-27 16:18:58

  Katika jangwa la Sahara, siafu wanatakiwa kusafiri jangwani kutafuta wadudu waliokufa ambao ni chakula chao. Jangwani kuna joto kali sana, inawabidi siafu hao warudi nyumbani kwa kasi ili wasife njiani.

  Utafiti wa zamani umethibitisha kuwa siafu wanarekodi hatua zao ili kupima umbali waliosafiri. Na ripoti mpya iliyotolewa kwenye tovuti ya gazeti la Sayansi inaonesha kuwa si kama tu wanapima umbali kwa kurekodi hatua zao, bali pia kwa macho yao. Njia yao ya kupima umbali ni kama tunavyokadiri umbali na mwelekeo kwa macho yetu tunapokuwa garini.

  Watafiti waliyafunika macho ya siafu kwa rangi ya njano, ili kujua kama wanaweza kurudi nyumbani au la bila kuona. Matokeo yanaonesha kuwa, siafu wanaotembea kwa miguu yao wanaweza kurudi nyumbani bila kuona, lakini siafu wafanyakazi waliokwenda mbali kwa kubebwa na siafu wengine hawawezi kurudi. Kama macho yao hayajafunikwa, basi ingawa hawajui siafu waliowabeba walitembea kwa hatua ngapi, bado wanaweza kurudi nyumbani kwa kupima umbali kwa macho yao. Hili ni jambo la kushangaza, kwani kabla ya hapo wanasayansi walifikiri macho yao hayawasaidii sana.

  Watafiti walisema mazingira ya siafu hao ni magumu sana, inawabidi kujifunza njia mbili za kupima umbali, yaani kuhesabu hatua na kuona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako