• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wakulima wahimizwa kutumia mbinu mpya kuivisha ndizi

    (GMT+08:00) 2016-09-29 21:08:11

    Wakulima katika kaunti ya Trans Nzoia nchini kenya wamehimizwa watumie teknolojia mpya ya kuivisha ndizi itakayowaongezea faida katika biashara ya tunda hilo.

    Naibu Gavana wa kaunti hioyo Dkt Stanley Tarus amewahamasisha wakulima waitumie teknolojia hiyo inayoitwa 'Banana Ripening Box' inayoivisha ndizi kwa siku tatu pekee badala ya siku saba au siku 14.

    Tarus alisema anataka wakulima watumie uvumbuzi huu mzuri badala ya kutegemea mbinu za zamani ambapo wakulima walitumia magunia ya kuivisha ndizi kwa muda mrefu au kemikali zinazodhuru afya.

    Aidha Dkt Tarus alisema kuwa serikali ya kaunti inaandaa mkataba wa makubaliano kati yao na kaunti ya Nandi ili wasambaze masanduku hayo ya teknolojia kwa wakulima wao wa migomba.

    Wakati huohuo Tarus amesema uvumbuzi huo utawavutia wakulima wao kupanda migomba pia badala ya kutegemea mahindi pekee ambayo hayaleti faida mno kwa sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako