• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuweka chakula kimoto kwenye friji kutaharibu friji?

  (GMT+08:00) 2016-09-30 10:43:20

  Watu wanatoa maarifa mengi kuhusu maisha ya kila siku. Inaonekana kwamba maarifa hayo yanasaidia, lakini ukweli ni kwamba mengi hayana msingi.

  Kwa mfano, baadhi ya watu wanaamini kuweka chakula kimoto kwenye friji kutaharibu friji. Huu ni uwongo.

  Chakula kimoto huwa na nyuzi 100 sentigredi. Joto likishuka na kufikia nyuzi 60, vijidudu vinaanza kukua. Katika joto la nyuzi 30 hadi 40, vijidudu vinakua kwa kasi zaidi. Joto likishuka zaidi na kufikia nyuzi 7, vijidudu vitaingia katika hali bwete.

  Hivyo kuweka chakula kwenye mazingira yenye joto chini ya nyuzi 7, yaani kwenye friji, kunasaidia kuzuia vijidudu visikue.

  Shirika la Afya Duniani limependekeza kutoweka chakula katika joto la kawaida kwa zaidi ya saa 2.

  Mafriji yanayotengenezwa siku hizi yanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Ingawa kuweka chakula kimoto kwenye friji kutasababisha lifanye kazi zaidi na kutumia umeme mwingi kidogo, lakini kazi hizi si nyingi sana, haziliharibu friji lako.

  Kwa ujumla, usiwe na wasiwasi kuweka chakula kimoto kwenye friji, inasaidia kuhakikisha usalama wa chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako