• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Roboti zinazotoa huduma zatumiwa zaidi siku hadi siku

  (GMT+08:00) 2016-09-30 10:43:38

  Maonesho ya vifaa vyenye akili na roboti yamefanyika hivi karibuni mjini Guangzhou, China. Siku hizi roboti zinazotoa huduma zinatumiwa zaidi katika mambo ya elimu, chakula, ulinzi, michezo, burudani na upashanaji habari.

  Vyombo vya umeme vya jikoni vyenye utambuzi vimewavutia watazamaji wengi. Ukibonyeza vitufe vichache tu, chombo cha kupika kitaweka viungo mbalimbali kwenye sufuria, na kupika chenyewe kwa mujibu wa mpango. Na chombo cha kugawanya wali kinaweza kuweka wali kwenye sahani, ambacho kinafaa kutumiwa kwenye kantini.

  Meneja mkuu wa idara ya vyombo vya kibiashara ya kampuni ya Deao Bw. He Jiangcheng alisema bei ya seti moja ya vyombo vya jikoni ni yuan elfu 60 hivi. Vyombo hivi vikitumiwa kwenye kantini, si kama tu vinasaidia kupunguza idadi ya wapishi, bali pia vinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na ninasaidia kuhakikisha kupika chakula safi. Hivi sasa viwanda na shule nyingi zimeagiza vyombo hivi.

  Roboti za kutoa elimu zimewavutia wazazi na watoto wengi. Watu wakisema maneno machache, roboti zinaitikia mara moja kwa kusema "Hujambo, unahitaji huduma gani?" Roboti hizi pia zinaweza kuimba, kusimulia hadithi, na kuonesha video za katuni.

  Lakini kwa sasa roboti zinazotoa huduma bado zina utambuzi wa kiwango cha chini, na zinaweza kufanya kazi rahisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako