• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Proteni mpya yatazamiwa kutengeneza dawa za kuua wadudu wa mahindi

  (GMT+08:00) 2016-09-30 10:43:55

  Ripoti mpya iliyotolewa kwenye gazeti la Sayansi la Marekani inaonesha kuwa proteni mpya iliyogunduliwa kwenye viumbe vidogovidogo vinavyoishi katika udongo inaweza kuua wadudu wanaoharibu mizizi ya mahindi kwa ufanisi mkubwa. Proteni hii inatazamiwa kutengenezwa dawa mpya za kuwaua wadudu badala ya dawa aina ya Bt.

  Dawa ya Bt ni dawa yenye Protini ya Bt inayotumiwa kwa wingi zaidi duniani. Protini hiyo inaweza kuwaua wadudu bila ya kudhuru afya ya binadamu, hivyo imetumiwa kwa wingi katika mashamba ya mazao yaliyorekebishwa jeni. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wadudu wamekuwa na uwezo wa kukinga dawa hiyo, hivyo kutafuta dawa mpya ni jambo muhimu. Mkurugenzi wa utafiti wa Kampuni ya DuPont Pioneer Lu Liu alisema wametenga viumbe vidogovidogo kutoka kwenye udongo unaosaidia kukinga wadudu wanaoharibu mizizi ya mahidi, na kugundua protini iitwayo IPD072Aa kutoka kwenye vijidudu aina ya Pseudomonas.

  Ili kupima uwezo wa kuwaua wadudu wa protini hiyo, watafiti walikuza mahindi yenye protini hiyo kwa kurekebisha jeni, halafu walipanda mahindi hayo na mahindi ya kawaida kwenye mashamba matano. Matokeo yanaonesha kuwa protini hiyo inaweza kuwakinga wadudu, hata wale wenye uwezo wa kukinga Protini ya Bt.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako