• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Ufisadi ndio donda sugu kwa ukuaji wa biashara Kenya.

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:53:34

    Kulingana na ripoti ya Baraza la Uchumi Ulimwenguni (WEF), ufisadi bado ni changamoto kuu kwa wafanyibiashara wa Kenya. Kulingana na ripoti iliyotolewa Jumatano, ufisadi unaoongoza kwa asilimia 17.8. Kikwazo kingine ni ushuru kwa asilimia 13.7, kisha ugumu wa kupata ufadhili wa uwekezaji kwa asilimia 11.5.

    Ripoti hii inaiorodhesha Kenya ya 96 kati ya mataifa 138 yaliyofanyiwa uchunguzi huu kuhusu mandhari ya kufanyia biashara.

    Kenya imepiga hatua ikizingatiwa kuwa mwaka uliopita, ilikuwa katika nafasi ya 99, na ufisadi uliogoza kwa asilimia 19.7.

    Uchunguzi wa ripoti hiyo vile vile unaonyesha kwamba Kenya iko katika nafasi nzuri ya kujiukuza kiuchumi siku za usooni kwa sababu ya kuwekeza sana kwenye nyanja za teknolojia na elimu.

    Mapendekezo ya ripoti hiyo ni pamoja na kuhimiza serikali na haswa sekta ya elimu kuwaelimisha wanafunzi jinsi ya kujitegemea kimaisha na isiwe tu kupita mitihani ya kitaifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako