Benki kuu ya China imesema kuwa China itaendelea kusukuma mbele mageuzi ya mfumo wa fedha na kufungua mlango zaidi kwa nje, baada ya sarafu yake RMB kuingizwa kwenye utaratibu wa SDR wa Shirika la fedha la kimataifa IMF.
Ijumaa iliyopita shirika la IMF lilitangaza kundi jipya la sarafu za SDR ikiwemo sarafu ya China Yuan, ambalo limeanza kufanya kazi rasmi leo, likisema kuwa hii ni hatua muhimu ya kihistoria kwa China, shirika la IMF na mfumo wa fedha wa kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na benki kuu ya China kwenye tovuti yake inasema, China inakaribisha hatua hiyo, ambayo itaimarisha uwakilishi, utulivu na mvuto wa utaratibu wa SDR wakati mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa yanapoendelezwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |