• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Man United yashindwa kuonesha ubabe mbele ya Stoke City, yalazimishwa sare

    (GMT+08:00) 2016-10-03 08:55:21

    Bado hali sio nzuri kwa upande wa kocha wa Man United na vijana wake Jose Mourinho, baada ya jana kushuka tena katika uwanja wake wa Old Trafford kucheza mchezo wa 7 wa Ligi Kuu England dhidi ya Stoke City. Klabu ya Stoke City ilijipatia pointi moja katika uwanja wa Old Trafford baada ya Joe Allen kusawazisha na hivyo basi kuiadhibu Manchester United iliyotawala mechi hiyo kwa kipindi cha muda mrefu. Baada ya kipa wa Stoke kuokoa mashambulio mengi katika kipindi cha kwanza cha mechi, United ilijiweka kifua mbele baada ya mchezaji wa ziada Anthony Martial kufunga bao la kwanza.

    Ilikuwa pigo kubwa kwa Stoke ambayo ilikuwa haijafanya shambulio lolote katika ngome ya United. Lakini baada ya Jon Walters kupiga krosi, Allen alifika na kusawazisha hivyo kuwafumba mdomo mashabiki wa United ambao walikuwa wakiimba katika kipindi chote cha mchuano huo. Stoke City ambayo iko katika nafasi ya pili kutoka mwisho sasa imejiongezea matumaini ya kuondoka katika eneo la mkia la ligi hiyo ya Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako