• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gareth Southgate awaita Lingard na Rashford kwenye kikosi cha timu ya taifa

    (GMT+08:00) 2016-10-04 09:06:50
    Winga wa Manchester United, Jesse Lingard, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England na kocha wa muda wa timu hiyo Gareth Southgate, kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Malta na Slovenia.

    Lingard, aliwahi kuitwa mara moja kipindi cha nyuma, lakini hakutumika kwenye mchezo wa England wa ushindi wa mabao, 2-0 dhidi ya Ufaransa katika mwezi Novemba mwaka uliopita.

    Mchezaji mwingine wa United, Marcus Rashford, ameitwa tena kwenye kikosi hicho cha wakubwa, baada ya kuonesha kiwango kizuri alipoifungia hat-trick, timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, dhidi ya Norway mwezi uliopita.

    Naye, mlinzi wa Stoke City, Glen Johnson ameitwa tena kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014, huku winga wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain akirejea baada ya kukaa benchi kwa muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako