Serikali ya China imetoa mpango wa ushirikiano kwenye maeneo ya sayansi na teknolojia kati ya China na nchi zilizoko kwenye Ukanda mmoja na Njia moja.
Kwa mujibu wa waraka wa serikali, katika kipindi cha miaka mitano ijayo China inapanga kuunda maabara za pamoja, vituo vya utafiti, vituo vya kubadilishana teknolojia na Bustani za sayansi na teknolojia katika nchi zilizopo kwenye Ukanda mmoja na Njia moja.
Serikali pia inalenga kuleta wafanyakazi wa zaidi ya laki moja na nusu wa sekta ya sayansi na teknolojia kutoka nchi hizo kwa ajili ya kubadilisha ujuzi au kupata mafunzo, na kutarajia kupata wanasayansi vijana zaidi ya elfu tano katika kipindi hicho.
Mpango wa Ukanda mmoja, Njia moja unahusu mpango wa kiuchumi wa njia ya Hariri na njia ya Hariri ya baharini ya karne ya 21, ambao ni mtandao wa biashara na miundo mbinu unaounganisha bara la Asia, Ulaya na Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |